top of page
DSC_0934.JPG

Lango la 26 Adari, Vol.2 (23 Mei, 2021) na 12 Ethanimu, VOl.2 (21 Novemba, 2021),

Kanisa lilifanya Mkutano Mbeya na Dar es Salaam kuhusu SURA HALISI YA KANISA NI IPI ? Katika Mikutano hii miwili, Kanisa lilisisitiza kupitia

I Timotheo 2:1-4 na Efeso 3:10; kwamba ni wajibu wa Kanisa kuinua Taifa, walioko madarakani na wananchi wote ili tusipatwe na majanga, milipuko ya magonjwa na adha za aina yoyote.

Kanisa liliweka wazi kuwa ni kosa kwa yeyote anayeitwa Mtumishi wa MUNGU Kulaumu Viongozi walioko Madarakani wakati yeye ndiye aliyepewa Uweza wa MUUMBA WA VOTE, WOTE NA YOTE kufuta mabaya katika jamii yanayotokana na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho. Pia Kanisa, liliweka wazi kuwa ukiona jambo lolote baya katika jamii limetokea na kudumu, basi ujue hiyo jamii haina Kanisa la kweli. Huo ndio ujumbe na msimamo wa Kanisa Halisi la MUNGU BABA.

DSC_0721.JPG
DSC_0489.JPG

Msimamo wa Kanisa ni kwamba, hatutakiwi kuchangia mijadala ya matusi na ile ya kurushiana madongo, bali tunatakiwa kuombea Taifa, Viongozi wake na Wananchi wake, ili MUUMBA WA VOTE, WOTE NA YOTE apate Barabara ya kuleta uponyaji katika Taifa. Kiongozi wa Serikali aliyeshiriki Mkutano wa Mbeya ni Mkuu wa Wilaya

bottom of page