BARUA PEPE: kanisahalisi@gmail.com | S.L.P 33070 DSM | Simu +255 (0) 719 341 327
Tegeta, Namanga, Kiwanja Na. 195
"Heri uliyekombolewa na CHANZO HALISI"
Kanisa lilifanya mkutano wa ufunguzi wa kitabu cha Ufahamu uliaoanzia Tanzania kwenda mataifa mengine, Katika ukumbi wa Arusha International Conference Center (AICC).
Mgeni Rasmi alikuwa ni Mkuu Wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V Mongela akiwa na viongozi wengine. Pia ulihudhuriwa na uzao wote wa KANISA HALISI ndani na nje ya Taifa Baba (Tanzania).
Kitabu cha Ufahamu Ulioanzia Tanzania Kwenda Mataifa Mengine kiliandikwa na Baba Halisi kwa takribani miaka mitano. Kikiwa hakitokani na elimu aliyosoma darasani, Ulaya, America, Afrika bali ni Sauti ya Aliyeumba yaani CHANZO HALISI ambayo iliyosikika kwake kwa mara ya kwanza 2015, 2019, na 2020. Pia Sauti hiyo anaisikia kila lango (siku) ikizidi kulihamisha Kanisa Kituo kila lango (siku) ndio imesababisha maandishi hayo.
Sababu kubwa ya Mkutano huu wa uzinduzi wa kitabu hiki ni:
1. Ni Utimilifu wa Math.21:43
Bwana Yesu miaka elf mbili iliyopita wayahudi walimuuzi hii ni dhahiri katika kitabu cha Yoh.9:28-29; Akawaambia kwakuwa mmeniudhi basi ufalme utahama kutoka mashariki ya kati utaenda kwenye Taifa lingine amabalo kwa kipindi kile hakulitaja, Ila tumekuja kugundua Taifa hilo ni Tanzania.
Kinachosababisha tutamke kwa ujasiri kabisa mahali pa wazi kama hapa mbele ya kila mmoja ni kwa kuwa, Israel ilisikika Sauti Ya MUNGU BABA ambae ndie CHANZO HALISI mara tatu (Musa, Eliya Mtishbi na Yesu) na Tanzania vile vile imesikika Sauti ya MUNGU BABA ambaye ndie Muumba Wa Kila Kitu Kizuri mara nne (2003 - Eliya Adamu II, 2015 - Miaka 1000, 2019 - MUNGU BABA na 2020 - CHANZO HALISI).
Na si kwamba Yesu alibahatisha kusema hivyo kwasababu ukiangalia:
A. Kwa Musa ambae ni Nabii mkubwa tunaemsoma kwenye Kitabu (. ) alioa Afrika, mpaka ikapeleka ndugu zake kumchukia kwasababu hiyo.
B.Lakini hata Yesu nae wakati Herode anataka kumuangamiza alikimbilia Afrika, lakini pia Bwana Yesu mwenyewe wakati ameelemewa na msalaba waliomsaidia kuubeba msalaba ni wa Afrika.
Na ndio maana miaka elfu mbili iliyopita alisema basi ufalme utahama kutoka mashariki ya kati, hakutaja wazi ili alinde taifa hilo kwa wakati ule ila leo tumegundua ni hili hapa baada ya Sauti kusikika mara nne.
Na wengi wanajiuliza je! jema linaweza kutokea Tanzania? basi leo limetokea; Wazungu wansema “Can the Cape be Of Good Hope? ” Then it has happened today.
2. Kweli kuhusu maana Halisi ya KANISA
Maana mara nyingi Kanisa huwa tunajua ni jengo lenye alama ya msalaba, lakini sisi tumepata Ufahamu tukagundua kwamba kumbe Kanisa ni mtu mwenye Moyo unaomjua Aliyeumba Kila Kitu. Tumepata Ufahamu kwamba Kanisa linapaswa kuwa Familia; Familia amabayo ina Baba, ina Mama na Ina Moyo mmoja na ndivyo tunavyoishi sisi KANISA HALISI. Lingine tumepata Ufahamu kwamba ndani ya Kanisa hapatakiwi kuwepo na Cheo kwasababu pakiwepo na cheo mnapigana na kukosoana kila wakati.
Na Familia hiyo ina mambo makubwa matatu;
❖ Inatakiwa ifundishe Amani,
❖ Ifundishe Upendo Usiobagua,
❖ Kuzalisha Mambo Mazuri.
Kanisa Halisi tunaishi ivyo kwa kufundisha mambo makubwa matatu;
-
Amani kwa kila mmoja unaekutana nae,
-
Upendo Usiobagua kwa kila mmoja,
-
Na pia kuhakikisha kila mmoja katika Familia anazalisha
vitu vizuri.
TAZAMA MKUTANO HUU ILI KUELEWA ZAIDI: https://www.youtube.com/watch?v=yP_O6C-g9D8