top of page

Lango la 26 Eluli, Vol. 1 (6 Desemba, 2020), Kanisa lilifanya uzinduzi wa "Ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda Mataifa mengine yote" (Mathayo 21:43). Vito vote vya Kanisa Tanzania vilishiriki uzinduzi huu pamoja na Vito vya Mataifa yaliyozunguka Tanzania kuthibitisha kuwa ufahamu huu ulioanzia Tanzania ni wa kweli. Wakati Ufahamu huu unazinduliwa, tulikuwa bado tuna Vitabu vitatu peke yake:

​

​

​

​

​

​

​

​

​

​

1. Kuvuka Mto usiovukika (Vol.1);

2. Kuingia Shamba Jipya (Vol.2); na,

3. Kuingia Mji wa Raha (Vol.3).

Sasa tayari tuna Kitabu cha Nne na cha Tano:

4. Kuingia Bustani Mpya (Vol.4); na, .

5. Kuingia Majira na Wakati Kabla ya Uharibifu (Vol.5).

​

​

​

​

​

​

​

 

​

 

Hii ni SAFARI YA UZAO WA MUNGU BABA kwa miaka Minne, kutoka Moyo wa Mwanzo kuingia kwa CHANZO HALISI, yaani Maisha bila mateso kwa kumtegemea MUUMBA WA VOTE, WOTE NA YOTE peke yake. Kitabu kilichoanza sasa hivi ni cha Sita, yaani SAFARI

YA UZAO WA MUNGU BABA kuingia Uwanja wa Moyo (Vol.6). Baada ya Vol.6, kitabu kinatakiwa kiunganishwe ili kiwe kimoja tu.

​

​

​

​

​

​

​

​

​

 

Thamani ya Ufahamu huu ulioanzia Tanzania kwenda mataifa mengine, ni mishale ya Ufahamu/Nuru kutoka Tanzania Afrika kwenda Mabara yote; tofauti na ilivyokuwa mwanzoni (mishale ya Ufahamu/Nuru ilivyokuwa inatoka Mashariki ya Kati kwenda mataifa

mengine yote).

20201206_140221.jpg
bottom of page