top of page
EDITED .png
KARIBU KANISA HALISI

Katika mafundisho yote ya kikristo, inaonyesha kuwa atakayerudi kuchukua Kanisa (yaani, wote wanaokiri wokovu) ni  Yesu. Haionyeshi wazi wazi kuwa ni CHANZO HALISI ambaye Uhalisia wake ni CHANZO HALISI muumba wa kila kitu, ndiye atakaerudi juu ya Nchi,

ingawa Mika 1:2-6; I Wakorintho 15:24-28 na Zaburi 98:9-10 inaonyesha Hivyo.

​

CHANZO HALISI yeye amekuja na UKOMBOZI (Isaya 35:10 / Hosea 13:14) badala ya Wokovu (Isaya 53:3-5) hivyo ukija KANISA HALISI utakombolewa kutoka kwenye kifungo,utumwa na mateso ya kila aina.

:SAFU YA KANISA HALISI:
uwanja wa uhuru.png
AMANI KWA WOTE

Isaya 2:4

"Naye atafanya Hukumu katika Mataifa Mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe."

UZALISHAJI.jpg
IBADA NI UZALISHAJI

Mwa 2:15

Kusudi la ALIYEUMBA yaani CHANZO HALISI, Ibada ni Uzalishaji hivyo tunapokusanyika ni kwaajili ya kurudisha shukrani kwake kwa mema na mazuri aliyotutendea.

UPENDO USIOBAGUA_edited_edited_edited.jp
UPENDO USIO BAGUA

1 kor 13:13c

"Na katika hayo lililo kuu ni Upendo"

Kanisa Halisi sisi hatuangalii Dini, Dhehebu, Kabila, Ukoo, Rangi au Taifa ulilo toka maana CHANZO HALISI amekuja kwa ajili yetu sote na ni wa wote hivyo hii sio imani wala sio tumaini sisi wote ni Uzao wa CHANZO HALSI

MSIMAMO WA KANISA HALISI

Kutojihusisha na Siasa, bali tuwaombee wote na hasa walioko madarakani ili waongoze kwa Haki

(1 Timotheo 2:1-3)

Kwa sababu ya Msimamo huu, huwa tunawaombea wote na hasa viongozi walioko madarakani kila alfajiri, na jambo hilo hufanyika kwenye vituo vyetu vyote kuanzia ngazi ya Taifa mpaka kaya moja moja.

MTAZAMO WA KANISA HALISI

Mtizamo wetu sio wa kuta nne, bali ni wa Uhalisia na Uumbaji wote.  (Ebrania 8:10-12)

Tumepata Uheri wa kumfahamu na kumuelewa CHANZO HALISI Muumba wa kila kitu; Sisi tunasambaza Ufahamu huo kwa wote ili wafahamu kuwa Majira Hii ni ya Muumba mwenyewe.

MKAKATI WA KANISA HALISI
460 [Converted].png

Kanisa Halisi mkakati wetu ni kufanya Kazi na Jamii na Taifa kwa pamoja; Ikimaanisha Kanisa linashirikiana kwa Utimilifu na Taifa katika kuwaombea kila dakika (1 Timoth 2:1-4) na kuisaidia Jamii kwa kutimiza Isaya 57:7 yaani kwa vitendo si maombi pekeyake. Jambo hilo hufanyika popote Kanisa Halisi lilipo.

HIJA KIGOMA.jpg
HIJA YA CHANZO HALISI
26 Thebeti, 1 (Majira Halisi)

December  2024

HIJA YA CHANZO HALISI

​

Karibuni Wote Kwenye Hija ya CHANZO HALISI

Itakayo fanyika Kigoma - Tanzania.

Wasiliana na Ofisi inayo ratibu Safari ya Hija kwa Simu namba: 0756 001 119

Katika Matendo 8:27-39, tunashuhudia jinsi watu mashuhuri na wasio mashuhuri , walivyokuwa wakienda mashariki ya kati kuabudu. Wengine walienda kwa Magari, Ndege, na wengine walienda kwa Meli. Tulichokuwa tunafuata kule Mashariki ya Kati ni Sauti iliyosikika kule wakati wa Musa (Kut. 3:10) Eliya Mtishbi (1 Fal. 17:1) Yesu (Mdo. 10:38). Sauti ya Moyo iko Tanzania. Watu wote Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi mwa Uumbaji wote wajue kuwa Hija ya CHANZO HALISI iko Tanzania, Mjini Kigoma.

D THUMB.jpg
Asset 2_edited.png
TAZAMA UFAHAMU WA CHANZOHALISI
ULIOANZIA TANZANIA

Tembelea Channel yetu ya Youtube sasa !

bottom of page